Skip survey header
Low Vision Mode Swahili

Wiki EARTH Utafiti wa Uwezo na Mahitaji

Mpendwa Mshiriki,

Utafiti huu unakusudia kuuliza juu ya uelewa kuhusu East African Regional and Thematic Hub (EARTH).

Hubs ni jina la Kikundi/Kitovu cha kishirika katika vuguvugu la Wikimedia kinachosaidia zaidi ya jumuiya moja ya kujitolea. Vitovu vinafikiriwa kuwa vya kikanda (kijiografia, k.m. Ulaya Mashariki ya Kati) na vya kimada. Vitakuwa ama uboreshaji wa jumuiya zilizopo, ushirikiano kati ya washirika, au miundo mipya iliyoundwa kwa madhumuni mahususi.

Wewe ukiwa kama mchangiaji wa miradi ya Wikimedia, umetambuliwa na kuombwa kushiriki katika utafiti huu ili kusaidia kamati ya uongozi ya EARTH, na jumuiya kwa ujumla kujibu maswali mawili yafuatayo:

  1. Ni maeneo gani ya mada ambayo unadhani HUB inapaswa kushughulikia?
  2. HUB inapaswa kuonekanaje katika ukanda wetu (km. Muundo wake uweje)
Kushiriki katika utafiti huu ni kwa hiari na hakutachukua zaidi ya dakika 15. Ikiwa huwezi kukamilisha utafiti kwa muda mmoja, majibu yako yatahifadhiwa ili uweze kurudi kwenye utafiti ukiwa na muda zaidi.

Utafiti utafungwa tarehe 1 Machi 2023.

Kwa kuendelea hadi ukurasa unaofuata, unakubali masharti ya kushiriki katika utafiti huu na umeelewa maelezo yaliyotolewa hapo juu na kwa hivyo unakubali kwa hiari kushiriki.

Tafadhali wasiliana na Wikimedia Community User Group Tanzania kama una swali lolote kuhusu utafiti huu kwa:  antonicmtavangu@gmail.com